NEW YORK  ,Marekani

 

MCHEKESHAJI Don Rickles,amewekwa chini ya ulinzi, baada ya kutoa kichekesho ambacho kinaonekana kumdhalilisha Rais Barack Obama kwa njia ya ubaguzi wa rangi.

Kwa mujibu wa mtandao wa Dital Spy, muigizaji huyo wa vichekesho alitiwa mbaroni mwishoni mwa wiki iliyopita wakati  tamasha lililoandaliwa na taasisi ya filamu ili kumpa tuzo  muigizaji, Shirley MacLaine.

Kwa mujibu  wa waandishi wa habari wa Hollywood ,muigizaji huyo alijikuta akiingia matatani baada ya kupewa nafasi ya kutoa neno kumpongeza,  MacLaine  ambapo alijikuta akitania akisema kwamba :”Mimi sipaswi kufurahi na watu weusi,Ila  Rais Obama ni rafiki yangu  na jana alikuwa nyumbani kwangu lakini sikumkaribisha..” 

Katika tamasha hilo Rickles anaripotiwa kuwashambulia pia nyota wengi akiwamo  Jack Nicholson  na kaka yake MacLaine, Warren Beatty.

Pia ilielezwa kuwa  alichukua muda akimponda  Jennifer Aniston, akidai  kuwa mwanadada huyo siku moja  alikimbia  meza yake  wakati wakiwa kwenye  mgahawa mmoja jijini New York  kwa sababu  alikuwa katikati ya  joto la  mashoga.

Advertisements