Ile kashfa ya Diamond kunaswa hotelini na mcheza sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel inadaiwa kuchafua vibaya upande wa wakwe zake Diamond.

Mtu wa karibu wa pande zote hizo mbili alisema: “Asikwambie mtu, unajua upande wa akina Jokate ni watu wa dini sana. Yaani kwa skendo skendo kama hizo, wanamuona Diamond kama anataka kuwachafua.

“Unajua zile ishu za kudaiwa kutoka kimapenzi na msururu wa wanawake zilikuwa zimeanza kutulia kwa sababu yupo na Jokate lakini baada ya kutokea hii ya kunaswa hotelini na Aunt, imetibua mambo kule ukweni na mbaya zaidi anaonekana hajatulia,” alimalizia mtu huyo ambaye hakutaka jina lake liwekwe hadharani

Baada ya habari hizo kutufikia tuliamua kumtafuta Diamond kuthibitisha juu ya hayo yaliyozungumzwa. Alipopatikanwa alikuwa na haya ya kusema: “Naomba niweke wazi jambo hili kwa sababu ni kweli nachafuliwa.

“Kuna watu wananichafua ili nionekane kituko kwenye familia ya akina Jokate, nahisi wanaweza kufanikiwa,” alisema Diamond.

Kufuatia ishu hiyo, uhusiano wa kimapenzi wa mwanamuziki huyo Diamond na mwanamitindo Jokate unadaiwa kuwa kwenye hatihati pamoja na kwamba bado wapo pamoja.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Diamond na Aunt walidaiwa kukutwa katika Hoteli ya Kebby’s iliyopo Mwenge, jijini Dar wakila ‘good time’, hivyo kuzua tafrani kwenye uchumba wa mwanamuzi huyo na Jokate.

Advertisements