Raia wa Misri wanajianda kushiriki katika uchaguzi wa kwanza huru tangu mapinduzi ya kiraia yaliomuondoa Rais Hosni Mubarak mamlakani miezi 15 iliopita.Wapiga kura milioni 50 watashiriki katika uchaguzi huu ambao usalama unapewa kipa umbele.

Baraza kuu la jeshi nchini humo ambalo lilichukuwa utawala baada ya mapinduzi ya kiraia mwezi wa Februari mwaka jana, limeahidi kuwa uchaguzi utakuwa wa huru na haki.

Nafasi ya urais imewavutia jumla ya wanasiasa 12, wenye itakadi kali za kidini, walio na msimamo wastani na mawaziri waliotumikia utawala wa aliyekuwa Rais Hosni Mubarak.

habari zaidi gonga hapa/read more click here…
Advertisements