*SITTA ADAI WANAOKIMBILIA HUKO NI MAGAMBA YEYE SI MMOJA WAO, LOWASSA AMSHANGAA LEMA, ASEMA KUHAMIA CHADEMA SI SIRI,


Waandishi Wetu
 
SIKU chache baada ya aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kuwataja mawaziri wawili na mmoja aliyewahi kuwa Waziri Mkuu kwamba, wameomba kujiunga na chama hicho cha upinzani, wawili kati yao wamejitokeza na kuzungumzia madai hayo.
 
Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambao walitajwa na Lema, jana kwa nyakati tofauti walibeza madai hayo.
 
Jumamosi iliyopita, Lema akiwa wilayani Sengerema, Mwanza alisema mawaziri watatu, akiwamo mmoja aliyewahi kuwa waziri mkuu wameiomba kujiunga na Chadema lakini mmoja kati yao amekataliwa na wengine mchakato wa kuyakubali maombi yao unaendelea.
 
Katika mkutano huo, Lema aliwataja mawaziri hao kwa jina moja kuwa ni Sitta, Lowassa na waziri mwingine ambaye tunahifadhi jina lake kwa kuwa hakupatikana jana kuzungumzia madai hayo.

Msimamo wa Sitta
Sitta alipuuza madai hayo akiyaita ya kitoto na kueleza kuwa kwa hadhi yake, hawezi kuomba kujiunga Chadema na kusubiri majibu kama amekubaliwa au la.

“Yaani mimi niombe kwenda Chadema halafu nikae kabisa huku nikisubiri wanijibu! Huo ni upuuzi na jambo hili haliwezekani na si kweli hata kidogo. Kama Lema kasema hivyo, basi huo ni utoto na siasa za kihuni,” alisema Sitta.

Sitta huku akicheka aliongeza: “Sasa nimeomba kwa nani na kwa njia ipi ya mdomo au maandishi? Mimi siyo gamba. Ni mtu mwadilifu siwezi kujiunga katika utaratibu wa kuchukua magamba ndani ya CCM.”

“Wao Chadema wanachukua tu kila mtu. Wakienda kwenye mikutano pia wanachukua tu watu, sasa hivi wanachukua magamba CCM. Mimi nawatakia kila heri katika kuchukua magamba CCM.”


Sitta alisema yeye ni mwanasiasa makini na mwadilifu hawezi kukaa chungu kimoja na magamba… Wanalofanya kuchukua magamba ya CCM ni faraja hata kwa Katibu Mkuu Wilson Mukama.”

Mbunge huyo wa Urambo Mashariki, alisema kuchukua magamba CCM ni sawa na mtu ambaye anakwenda kwa jirani ambaye nyumba yake imezungukwa na takataka kisha akamsaidia kuzisomba kwenda kuzitupa… Hapo si lazima ufurahie bwana?
habari zaidi gonga hapa/read more click here…
Advertisements