Balozi Ryan Crocker wa Marekani nchini Afghanistan amethibitisha kuacha kazi kutokana na sababu za kiafya.
 
Taarifa za kidiplomasia zimesema kuwa balozi huyo anaachia nafasi hiyo kwa hiyari yake na si kutokana na shinikizo kama inavyodhaniwa.
 
Shirika la Habari la Reuters limekaririwa likisema kuwa Crocker ambaye ni mwanadiplomasia mkongwe aliyechukua jukumu hilo baada ya kustaafu, anatarajia kuondoka nafasi hiyo wakati huu ambapo Marekani inajiandaa kuondoa vikosi vyake vya kulinda amani nchini Afghanistan.
 
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani Victoria Nuland amesema kuwa Naibu wa Crocker, James Cunningham ndiye atakayechukua jukumu la kuendesha ubalozi huo kwa sasa lakini hakutaja mtu atakayechukua nafasi hiyo moja kwa moja.
 
Habari kwa hisani ya dewjiblog.com
Advertisements