NEW YORK,Marekani
 
IMERIPOTIWA kuwa maisha na kazi ya aliyekuwamwanamuziki mahili Whitney Houston,zitaenziwa wakati wa tamasha lijalo la  VH1 Divas.
 
Tamasha hilo ambalo ushuhudiwa baadhi ya wanbamuziki wa kike vinara dunia wakishirikiana kwa mwaka huu.litamuenzi marehemu nyota huyo wakati kipindi hicho kitakaporekodiwa baadaye mwishoni mwa mwaka huu.
 
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Marekani  AP, Muongozaji wa muziki wa Houston,Rickey Minor,ameshaandaa mtayarisha filamu maalumu ambaye ataanda afilamu hiyo itakayofanyika mjini Los Angeles,Desemba mwaka huu.
“Sote tunadhani kama kuna tamasha lolote lakuenzi muziki wa  Whitney,basi ni la  Divas,” alisema Rais  wa VH1, Tom Calderone. “Desema tunadhani ndiyo siku  muafaka ambapo kila mmoja hatasononeka kwani tunakuwa tunashilikiana kushrehekea muziki.
 
 
Wakti wa enzi zake Houston alionekana katika tamasha hilo la VH1 Divas,mara tatu mwaka  1999, 2002 na  2003 na katika miaka ya hivi karibuni imekuwakishuhudiwa wasanii kama  Mariah Carey, Beyoncé, Kelly Clarkson, Adele, Leona Lewis  na  Nicki Minaj.

Advertisements