NEW YORK,Marekani
 
TETESI za kwamba mwanamuziki  Lady GaGa,amevalishwa pete ya uchumba zimezidi kusambaa, baada ya kuonekana picha zinazomuonesha akiwa amevaa pete ya uchumba.
 
Kwa mujibu wa mtandao wa Digital Spy  picha hizo zilizoonekana kupitia katika tovuti ya  mpiga picha maarufu   Terry Richardson,ambapo  muimbaji huyo anaonekana  akionesha kidole kilichovalishwa pete ya uchumba.
 
Kuonekana kwa picha hizo kunadaiwa kuzua tetesi zinazomuhusisha  na kuvalishwa kwa pete hiyo.
 
Hata hivyo vyanzo vya habari vilivyopo karibu na  GaGa viliuambia mtandao wa  TMZ  kwamba nyota huyo hakuvalishwa pete ya uchumba na pete hiyo haina maana yoyote.
 

 

 

Advertisements