Hadija Kopa na wasanii wa muziki wa Bongo fleva, Ali Kiba, Omy Dimpoz, Roma Mkatoliki AT, pamoja na wakali wa Ragge Warriors walikonga vilivyo nyoyo za mashabiki wa burudani mjini Moshi na kudhihirisha uhalali wao wa kutwaa Tuzo mbalimbali za Kili Music 2012. Zifuatazo ni picha mbalimbali za tukio hilo.
 
Pichani juuni Mkali wa Bongo Fleva, Ali Kiba akiimba jukwaani hii leo wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award iliyofanyika kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro jana.
 
Barnaba Boy ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume akimbo jukwaani hii leo wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro jana.
 
  
DJ Choka akisugua vyombo kuendanda na Roma Mkatolik, picha ya pili kulia Roma Mkatoliki akitumbuiza jukwaani wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award mkoani Kilimanjaro.
 
Hapa ni usiku
 
Ni ……mchana
 
Aaanastua…huyu ni Gwiji Hadija Kopa akifanya vitu vyake jukwaani hapo Ushirika. Mama alifunika mbaya katika show hii
 
Wakali wa ragge kutoka kundi la Warriors from East la mjini Arusha wakitumbuiza mashabiki katika tamasha maalum la Washindi wa Kili Music Award 2012 kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro jana.
 
Msanii AT kutoka Zanzibar akitumbuiza jukwaani na wacheza sho wake wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro jana.
 
Kwa picha zaidi tembelea Mrokim.Blog
Advertisements