Image

NYOTA wa filamu za ‘Misuko Suko’ amabayo ilionekana kuwa na mguzo kwa  na kuteka mashabiki lukuki hatimaye hali iliyosababisha itolewe kuanzia toleo la
kwanza hadi la tatu kwa kipindi cha nyakati tofau.

Kupitia filamu hizo ambazo zinaubabe mwingi kwandi ndai ya filamu hizo  kuna mijeba yenye maumbile ya ‘Inglish-Body’ na kuna heka heka za kibabe ambazo
zimeijengea filamu ya ‘Misuko Suko’umaarufu mkubwa.

Mtayalishaji wa filamu hizo Jimmy Mponda ‘Jimmy Master’ anayomengi tu ya kutiririka katika makala hii.

Anasema alianza sanaa kwa kujihusisha na mchezo wa sarakasi , mwaka 1978 hadi
kufikia mwaka 1980 alijiunga na kikundi cha Yusta ambacho kilijihusisha na Sarakasi ngoma na maigizo ya Stejini.

Mwaka 1986 alianza kujihusisha na biashara na wakati huo huo akaanza pia kujihusisha na mchezo wa mapigano na Sarakasi akiwa mkoani Arusha (YMCA).

Kwa kuwa elimu ni kama nguzo ya kumuongoza mwanadamu kumudu mazingira yanayomzunguka Mponda anasema alisoma shule ya msingi na sekondari Arusha amabpo mwaka 1986 ndio mwaka alimaliza
kidato cha nne mkoani  Arusha.

Mwaka 1999 alikuja Dar , na mtazamo wake aliuhamishia Dar  mwaka 1989 hadi 1990 mwishoni.

Akiwa jijini Dar alikuwa akifanya biashara ya kupeleka bidhaa mbali mbali
mikoani.

Mwishoni mwa mwaka 1990 , aliamia mkoni Taanga ambapo alifanya biashara na mazoezi.

Akiwa katika pilika pilika za kibiashara alikutana na wenzake wengine na kuanzisha kundi lililoitwa (Black Ninja Group), ambapo walianza kujihusisha na
uandaaji wa shoo za mapigano.

Walianza kuipenyeza sanaa yao hiyo kwa kuvuka mipaka ya nchi za Kenya na Uganda ikiwa ni   mwaka 1992 hadi 1993.

Ambapo mwaka 1994 walipata wazo la kufanya filamu, walitaufuta mtunzi wa kuchukua matukio ya video na kuandaa fialmu ya ‘Shamba Kubwa’.

Filamu hiyo baada ya kukamilika waliweza kufanya uzinduzi kwenye mikoa ya Tanga , Mwanza na Iringa.

Kuanzia hapo Jimmy Master alibakiza asilimia 60 katika kufanya masuala ya filamu na asilimia 40 akazibakisha kwenye mawazo ya biashara.

Anasema ,”Filamu iliyofuata ilikuwa ikiitwa ‘Unga Adui wa Haki’ ilizungumzia
madawa ya kulenya.

“Ilikuwa mwaka 1996 ambapo mwaka uliofuata nilirudi tena jijini Dar es Salaam , nikitokea Tanga ambapo ndipo nikawa nimehamia jijini hapa moja kwa moja,”alisema Jimmy Master.

Mwaka 200 anasema aliandaa filamu iliyoitwa ‘USIA’ ambapo akujivika huusika wowote licha ya yeye kuwa
muhusika.

Hapo alifanikiwa kuibua vipaji mbali mbalivya Wasanii katika muziki wa Bongofleva .

Licha ya kujipatia umaarufu awali kwenye filamu ya ‘Shamba kubwa’ filamu ya ‘Misuko Suko’ iliyotoka mpaka matoleo
matatu ndio iliyokuza zaidi umaarufu na mafaniko yake mengi katika tasnia
hiyo ya filamu.

“Kunamafaniko lukuki amabyo ninayaona kwa sasa baada ya kutoa matoleo hayo ,
ambapo niliweza kupata ‘Ma-msapu’ na kufunga ndoa .

“Kwa sasa mie ni baba wa watoto wawili, na pia nimeongezea kuwa mjasiliamali, namiliki duka   linalojihusisha na huuzaji wa filamu karia koo likiuza
filamu mbali mbali na vifaa vya video Production namengineyo,”alisema Jimmy Master.

Alisema pia kwa sasa tayari ameingiza sokomi filamu mpya iitwayo ‘Doble J’ikiwa   imeandaliwa na kampuni yake
iitwayo ‘Jimpowood Campani LTD ,inayo patikana maeneo ya DDC Magomeni jijini
Dar es Salaam.

Anasema kuwa mafanikio mengine aliyoyapata kwa hivi sasa kwenye tasnia hiyo ya filamu ni kumiliki gari ainaya
Toyota Mark 11 lenye thamani ya milioni
16.

Msanii huyo anasema pia baadhi ya matukio ambayo sirahisi kuyasahau maishani mwake ni kuwa alishafiwa na mama yake mzazi , ambapo katika maisha
anasema mama huwa nguzo duniani

“Mama alifariki dunia nikiwa bado naitaji nasaha zake lakini mungu alimpenda zaidi.”

Pia msanii huyo nakumbuka zaidi tukio lililo wahi kumtukia la kupatwa na ajari mbaya ya gari maendeo ya Bia ramuro mkoani Kagera mwaka  1998 ambapo gari lilipinduka zaidi ya mara nne lakini mungu alisaidia akatoka salama

 

Advertisements