Baba yake na marehemu akitoa heshima za mwisho

 Mama yake na marehemu

 Mwili wa marehemu ukiwekwa kwenye gari tayari kusafirishwa kuelekea Goba

 Waheshimiwa wabunge,John Mnyika na Idd Azan leo kwenye kutoa heshima za mwisho.

 
WATU mbalimbali leo wamekusanyika katika Kanisa la Anglicana, Ubungo, jijini Dar es Salaam, kuuaga mwili wa marehemu, Rachel Mwiligwa aliyekuwa mhariri wa gazeti la Mtanzania na aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Alhamisi wiki iliyopita  katika hospitali ya Mwananyamala.  Alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya mapafu.
Waliohudhuria ni pamoja na wabunge, wasanii wa muziki na waandishi wa habari ambapo mwili huo uliwasili kanisani  saa 5:30 kabla ya kupelekwa kuzikwa nyumbani kwao Goba jijini Dar.
                             HABARI/PICHA NA GLADNESS MALLYA, GPL
Advertisements